Saturday 13 August 2016

Sunday 24 July 2016

PET BOY & MAN DVD & GUNJU MASTER TUNAVYOFANYA (OFFICIAL VIDEO)

PATA FURSA YA KUANGALIA WIMBO MPYA WA PET BOY UITWAO TUNAVYOFANYA



ANGALIA HAPA KISHA TOA MAONI YAKO

KUUTAZAMA ANGALIA HAPA





Diaspora

Tuesday 22 March 2016

MJASILIAMALI KATABI MAYUNGA.

Email: diasporagrouptz@gmail.com                                                                               MJASILIAMALI.


MOTTO: VIJANA NA KAZI
**********************************

Anaitwa KATABI MAYUNGA ni mjasiliamali wa siku nyingi, amefanya kazi mbalimbali katika maeneo tofauti tofauti.
Ni mwenyeji wa Jijini Mwanza, akiwa anafanya kazi kama CHINGA.
 
Amejiunga na DIASPORA COMPANY LTD na sasa ameboresha biashara yake baada ya kujitanua zaidi kwa kuongeza mahitaji ya wateja wake.
Unaweza kupata Bidhaa zake kiurahisi Zaidi popote pale Tanzania
Bidhaa mbalimbali kama zinavyoonekana hapa.

                                                       




KATABI MAYUNGA
Phone No: +255768234787
Facebook: Katabi Mayunga
Email:       diasporagrouptz@gmail.com 

Saturday 19 March 2016

KILIMO CHA TIKITI MAJI

KILIMO CHA TIKITI MAJI

Email: diasporagrouptz@gmail.com                                                          KILIMO CHA TIKITI MAJI
MOTTO: VIJANA NA KAZI
**************************************
            UTANGULIZI                   
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi.  Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa.  Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama  matango,maboga na maskwash.  Zao la tikiti maji  ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.

Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa  na kuhudumiwa  vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.


HALI YA HEWA
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.  Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi.  Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua:  kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.

HALI YA UDONGO
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile  haihitaji udongo wenye  kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0

MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA MATIKITI MAJI TANZANIA.
Kwa upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM, Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu  mpaka wa tisa.

UANDAAJI WA SHAMBA
Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingne ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonja.

UPANDAJI
Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja  katika kila  shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi  na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
UPUNGUZAJI WA MIMEA
Mimea ya matikitimaji huanza kuota, baada ya kama wiki 2. Hivyo  katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio uendelee kukua.
Angalizo: using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
 Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda.
Wakati  mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.


MATANDAZO (MULCHES)
 Matandazo ina maana ya kutumia  nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche  kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu  kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.

UWEKAJI WA MBOLEA
 Mbolea za viwandani aina ya NPK au mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10 hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni midogo mpaka pale maua ya kike yatakapoanza kuonekana.  Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya urea na potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.

UMWAGILIAJI
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache.  Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.
Angalizo; usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.

MAUA NA MATUNDA
 Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume  huwa  ni madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k
Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono. 
Hii hufanywa kwa, kukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.

MAGONJWA NA WADUDU
 Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti ugonjwa magonjwa hayo hapo juu.
Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda. Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.

MAVUNO
Mavuno ya matikiti yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Matikiti  pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya matikiti. Kwa wastani matikiti yanaweza kutoa kutoa mavuno kati ya TANI 15-36 kwa hekta moja. Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi.
SOKO LA MATIKITI MAJI
Ukubwa wa tikiti na mwonekano wake ni baadhi ya sifa zinazoangaliwa na wananuzi. Matikiti madogo sana huwa hayapendi sana na wanunuzi. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza matikiti katika masoko ya ndani yanayopatikana takribani nchi nzima. Kwa miaka kadhaa tikiti moja limekuwa  likiuzwa kwa wasitani wa shilling 1000 kwa tikiti  dogo mpaka 3000  kwa tikiti kubwa katika masoko.
Mwisho

UKITAKA UTAJIRI UTAUPATA SHAMBANI

Diaspora Company Ltd